1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu takriban 11 wauwawa kwenye shambulio la bomu Colombo

3 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D1jZ

Watu wasiopungua 11 wameuwawa na wengine 100 kujeruhiwa leo katika shambulio lililofanywa kwenye kituo cha treni mjini Colombo nchini Sri Lanka.

Mshambuliaji mwanamke wa kundi la waasi la Tamil Tigers kutoka kitongoji cha Ambepussa amejilipua nje ya treni wakati abiria walipokuwa wakishuka.

Shambulio hilo limefanywa licha ya usalama kuimarishwa nchini Sri Lanka huku nchi hiyo ikijiandaa kuadhimisha miaka 60 ya uhuru hapo kesho.

Kufikia sasa hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na shambulio hilo.

Mapema leo watalii sita walioitembelea bustani ya wanyama nje ya mji wa Colombo walijeruhiwa baada ya kushambuliwa kwa grenedi.