Watu hamsini wauwawa kwenye ajali ya treni Pakistan
19 Desemba 2007Matangazo
ISLAMABAD
Takriban watu hamsini wameuwawa wakati treni ilipoacha njia mapema leo hii kusini mwa Pakistan.
Ajali hiyo imetokea wakati mabebewa 14 kati ya mabehewa 16 ya treni hiyo ya abiria kutoka Karachi kwenda Lahore yalipoacha njia.
Polisi na watu wa kujitolea wanakimbilia eneo hilo lilioko kama kilomita 400 kusini mwa Karachi kuwaokowa wahanga ambapo inaripotiwa kwamba baadhi ya abiria wamenasa kwenye mabehewa ya treni.