Watu 47 wauawa Syria
17 Septemba 2011Matangazo
Kama raia 21 waliuawa katika wilaya ya Idlib karibu na mpaka wa Syria na Uturuki.
Kwa mujibu wa wanaharakati hao wa upinzani, vikosi hivyo vilikuwa vikifyatua risasi ovyo na wenyeji hawakuweza kuwasaidia majeruhi.
Wengine 6 waliuawa Hama na vifo vingine vilitokea mji mkuu Damascus, Homs na Deir al-Zour.
Ripoti hizo haziwezi kuthibitishwa na vyombo huru vya habari kwani serikali ya Syria imewapiga marufuku waandishi wa habari wa kigeni.