1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Watu 20 wafariki katika maporomoko ya udongo China

Amina Mjahid
23 Januari 2024

Watu 20 wamekufa baada ya maporomoko ya udongo kuangukia katika nyumba kadhaa kwenye kijiji kimoja kusini magharibi mwa mkoa wa Yunnan nchini China.

https://p.dw.com/p/4ba8P
China | Mapromoko ya udongo Yunnan
Jumla ya watu 47 walifunikwa na matope kusini-magharibi mwa mkoa wa Yunnan nchini China, kufuatia mafuriko yaliotokea Januari 22, 2024.Picha: Zhou Lei/Xinhua/picture alliance

Kulingana na shirika la habari la Xinhua tumu ya uokozi hadi sasa imefanikiwa kutoa miili 20 chini ya vifusi vya nyumba hizo. Bado shughuli ya kuwatafuta manusura wa mkasa huo inaendelea.

Soma pia: Maporomoko ya ardhi yaua watu zaidi ya 150 nchini Myanmar

Serikali ya China imesema bado watu 24 hawajulikani waliko baada ya kupungua kutoka 47 hapo jana. Nyumba takriban 18 zilizoko katika kijiji cha Liangshui kilichoko kaskazini mashariki katika mkoa wa Yunna zilifunikwa na udongo.

Serikali ya China imetuma mamia ya waokoaji na wanajeshi katika eneo la ajali. Takriban wakaazi 200 wameondolewa katika eneo hilo.