1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 12 wauwawa mjini Mogadishu

31 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CiWX

Watu takriban 12 wameuwawa kwenye mapigano makali yaliyozuka nchini Somalia. Miongoni mwa waliouwawa ni mama mmoja pamoja na watoto wake wadogo watano.

Maafisa na wakaazi wa mjini Mogadishu wanasema mapigano hayo yaliyozuka jana jioni yameelezwa kuwa mabaya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha mwezi mmoja.

Machafuko yalitokea kusini na kaskazini mwa mji mku Mogadishu kati ya wanajeshi wa serikali ya mpito ya Somalia wanaoungwa mkono na majeshi ya Ethiopia na wanamgambo wa kiislamu, mwaka mmoja tangu Ethiopia ilipotuma ndege zake za kivita na vifaru kulifukuza kundi la wanamgambo wa kiislamu ambalo lilikuwa likiudhibiti mji wa Mogadishu.