Watu 11 wauwawa katika mapigano makali Mogadishu.
8 Juni 2008Matangazo
Kwa mujibu wa mashahidi vikosi vya serikali vikiiungwa mkono na vile vya Ethiopia vilifanya msako katika mtaa wa Wardhigley kusini mwa mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu na kuzusha mapigano ambapo mahasimu walishambiliana kwa kutumia silaha nzito
Waethiopia walifyetua mizinga katika soko la Bakara ambapo inaelezwa kwamba raia wengi waliuwawa.Wanajeshi watatu wa Somalia na mwanamgambo mmoja wameuwawa katika kitongoji cha karibu cha Hararyale ambapo mpigano yaliwa makali sana.
Vikosi vya Ethiopia na vya Somalia pia vimekuwa vikitumia silaha za kutungulia ndege katika mapigano hayo.