1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watoto watumika kama wanajeshi.

24 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cfdp

Kinshasa.

Katika muda wa wiki chache zilizopita , watoto wameonekana wakifanya gwaride katika jimbo lililokumbwa na machafuko la mashariki katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo, wakati uandikishaji wa wanajeshi watoto unaofanywa na wapiganaji umefikia kiwango cha juu kabisa.

Taarifa iliyotolewa na shirika lisilo la kiserikali la okoa watoto, imesema leo kuwa hali kwa watoto mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo imefikia kiwango cha maafa. Wapiganaji kutoka pande zote wanawatumia watoto kama ngao, amesema Hussein Murshal , mkurugeni wa kundi hilo la kimataifa la kutoa misaada nchini Kongo.

Mapigano katika jimbo lenye matatizo la mashariki yameongezeka kwa kiwango kikubwa tangu mwezi wa August, wakati makundi hasimu ya waasi yakipigana katika maeneo ya misitu.