1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Watano wauwawa katika shambulio mjini Liege

Mtu mmoja aliyekuwa na maguruneti pamoja na bunduki ameshambulia soko la krismass katika mji wa Liege nchini Ubelgiji jana , na watu wanne pamoja na yeye binafsi kuuwawa.

Mtu mmoja aliyekuwa na maguruneti pamoja na bunduki ameshambulia soko la krismass katika mji wa Liege nchini Ubelgiji jana , na watu wanne pamoja na yeye binafsi kuuwawa. Watu 123 wamejeruhiwa katika shambulio hilo lililotokea jana mchana. Polisi imesema kuwa mtu huyo mwenye umri wa miaka 33 alirusha maguruneti matatu ya kutupwa kwa mkono katika soko hilo kabla ya kufyatua risasi katika kundi la watu. Polisi haijatoa taarifa mara moja juu ya kile kilichomshawishi mtu huyo kufanya shambulio hilo, ambaye aliwahi kuhukumiwa kifungo kwa kuwa na silaha. Afisa wa wizara ya mambo ya ndani hata hivyo amesema kuwa huenda ni shambulio la kigaidi. Mtu huyo alikuwa ameitwa kuhojiwa na polisi jana asubuhi lakini hakutokea. Hakuna anayefahamu hata hivyo mtu huyo aliuwawa vipi.

 • Tarehe 14.12.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13SFq
 • Tarehe 14.12.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13SFq

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com