Wasudani 2 wapigwa Dresden
23 Desemba 2007Matangazo
DRESDEN:
Polisi nchini Ujerumani imearifu kwamba wasudani 2 wamepigwa katika shambulio la chuki za kikabila na watu 5 waliowahujumu nje ya Disco 1 mjini Dresden,mashariki mwa Ujerumani.
Kijana wa kijerumani aliejaribu kuingilia kati kuzima mapigano alihujumiwa.Hakuna aliepata majaraha makubwa.