1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasomali 75,000 wakimbia makaazi yao

Daniel Gakuba
25 Oktoba 2016

Zaidi ya watu 75,000 wameyahama makaazi yao nchini Somalia kutokana na ghasia zilizodumu kwa wiki tatu, huku Umoja wa Mataifa ukisema wanawake na watoto wanalala nje wakati msimu wa mvua ukikaribia.

https://p.dw.com/p/2Rg6u
Somali Äthiopien Shinile-Zone Dürre erschwert Lebensbedingungen
Picha: J. Jeffrey

Ghasia hizo zilizuka Jumamosi na Jumapili katika mji wa Galkayo zikiwahusisha wapiganaji watiifu kwa mikoa miwili hasímu yenye mamlaka ya ndani, Puntland na Galmudug.

Ofisi ya Uratibu wa Misaada ya Umoja wa Mataifa (OCHA) inasema hofu kwamba ghasia hizo zinaweza kuendelea kwa muda mrefu, zinawafanya watu kuyakimbia maskani yao.

Mji wa Galkayo, ambao ni makao makuu ya mkoa wa Mugug, unakaliwa na koo zinazounga mkono mikoa miwili inayopingana.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imesema serikali kuu ya mjini Mogadishu inachukua hatua kurejesha utulivu.

Nchini Somalia, mmoja kati ya kila watu 10 ameyakimbia makaazi yake akiepuka machafuko.