1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Mafuriko yahofiwa Sudan kufuatia shambulio katika bwawa

18 Novemba 2023

Jeshi la Sudan na wanamgambo wa Rapid Support Forces RSF leo wamelaumiana kwa shambulizi lililoharibu daraja katika bwawa la Jebel Awlia kusini mwa Khartoum.

https://p.dw.com/p/4Z82c
Sehemu ya mji mkuu wa Sudan, Khartoum
Daraja la Mek Nimir linalopita katika mto Nile nchini SudanPicha: Ashraf Shazly/AFP/Getty Images

Ukubwa wa uharibifu uliofanywa katika bwawa hilo bado haujabainika ila uharibifu mkubwa unatishia kusababisha mafuriko. Hivi karibuni mapigano yameongezeka katika eneo la Jebel Awlia, wilaya ya kimaskini kusini mwa jimbo la Khartoum na kusababisha maelfu ya watu kuachwa bila makao.

Soma zaidi: Mapigano yaharibu daraja muhimu Khartoum

Mapema mwezi huu RSF ilisema imeiteka kambi ya jeshi katika eneo hilo. Katika wiki za hivi karibuni, daraja moja katika Mji Mkuu Khartoum na hifadhi muhimu ya mafuta viliharibiwa kwa mashambulizi na pande hizo mbili zikalaumiana vile vile kwa mashambulizi hayo.