WASHINGTON:Uchaguzi wa Bunge Marekani kuanza leo | Habari za Ulimwengu | DW | 07.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON:Uchaguzi wa Bunge Marekani kuanza leo

Uchaguzi wa bunge nchini Marekani unaanza leo.

Wanachama wa Republican na Demokrats walikuwa mbioni hapo jana kuwahamasisha wafuasi wao katika kampeini ya dakika za mwisho.

Rais Gorge W bush amekuwa akifanya kampeini katika majimbo ya kusini ya Florida,Texas na Arkansas.

Wademokrats wanalenga zaidi kampeini yao katika suala la Iraq na kujipa matumaini ya kushinda kutokana na jinsi utawala wa rais bush unavyokabiliwa na hali ngumu pamoja na jinsi unavyolishughulikia suala la Iraq.

Uchunguzi wa maoni ya watu uliofanywa hivi karibuni unaonyesha kuwa chama cha Demokrat huenda kikashinda tena udhibiti wa bunge la wawakilishi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com