WASHINGTON:Bush atishia vikwazo dhidi ya Sudan? | Habari za Ulimwengu | DW | 19.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON:Bush atishia vikwazo dhidi ya Sudan?

Rais George Bush amesema kuwa Marekani itaiwekea vikwazo Sudan ikiwa haitaruhusu jeshi kubwa la Umoja wa Mataifa kuingia katika jimbo la Darfur.

Rais Bush amesema amempa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa fursa ya mwisho ili afikie suluhisho la kidiplomasia na Sudan.

Hatahivyo mapema wiki hii serikali ya Sudan ilisema itawaruhusu askari alfu 3 wa Umoja wa Mataifa kungia katika jimbo la Darfur ili kuwaunga mkono askari alfu saba wa jeshi la Umoja wa Afrika wanaolinda amani katika jimbo hilo.

Lakini Sudan inapinga idadi kubwa zaidi ya askari wa Umoja wa Mataifa kuingia katika sehemu hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com