1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington:Baraza la Senate la Marekani linakataa kuuzungumzia mpango wa Rais Bush wa kupeleka majeshi zaidi nchini Iraq

18 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCR2

Baraza la Senate la Bunge la Marekani limekataa kuuzingatia mswada unaoulaani mpango wa Rais George Bush wa kupeleka majeshi zaidi nchini Iraq. Jambo hilo limefanyika siku moja kabla baraza la wawakilishi la bunge kuulaani mpango huo. Kwa mara ya pili mnamo wiki mbili, maseneta wa Chama cha Democratic wameshindwa kuukiuka ukaidi wa wabunge wa chama cha Republican ili kupata kura za kutosha kuweza kuzungumziwa hatua isiokuwa ya lazima ya kuupinga uamuzi wa karibuni wa Rais Bush wa kutuma wanajeshi 21,500 hadi Iraq. Wafuasi wa Rais Bush wanasema kutoengeza idadi ya wanajeshi katika Iraq kutawezesha uasi uengezeke katika nchi hiyo.