1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Watu tisa wauwawa katika mashambulio ya risasi

Watu takriban tisa wameuwawa katika visa viwili vya mashambulio ya risasi nchini Marekani. Watu watano wameuwawa katika kisa cha kwanza kilichotokea kwenye duka kubwa mjini Salt Lake wakati mwanamume mmoja alipoanza kuwafyatulia risasi wateja waliokuwa wakinunua bidhaa ndani ya duka hilo.

Polisi wanasema maofisa wa usalama waliingia ndani ya duka hilo na kumpiga risasi na kumuua mwanamume huyo.

Katika kisa cha pili, mwanamume mwingine aliwapiga risasi na kuwaua watu watatu wakati wa mkutano kuhusu maswala ya biashara huko Philadelphia. Polisi wanasema mwanamume huyo hatimaye alijiua mwenye kwa kujipiga risasi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com