1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Wakuu wa majeshi wataka mwelekeo mpya Iraq

14 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCjM
Watu wakioiga kura katika mji wa Port Harcourt nchini Nigeria hapo Jumamosi.
Watu wakioiga kura katika mji wa Port Harcourt nchini Nigeria hapo Jumamosi.Picha: AP

Wakuu wa kijeshi nchini Marekani wanapendekeza kwamba Rais George W. Bush abadili mweleko wake wa kijeshi nchini Iraq badala ya kupambana na waasi imarishe asasi za nchi hiyo.

Gazeti la Washington Post limeripoti leo hii kwa kukariri duru zenye uhusiano na Uchambuzi wa sera ya Iraq wa Ikulu ya Marekani kwamba wakuu hao wa majeshi hawapendelei kongezwa kwa vikosi nchini Iarq na kwamba rasilmali zaidi zinahatajika kuendeleza upatanishi wa kisisasa na ujenzi mpya wa kiuchumi hususan mpango wa ajira mpya.

Wakati huo huo Rais George W. Bush wa Marekani amesema hatoharakishwa katika kufanya mabadiliko makubwa ya mkakati wake kwa Iraq.

Kauli yake hiyo inafuatia uamuzi wake wa kuchelewesha kutangaza mweleko huo mpya hadi wakati wa Mwaka Mpya licha ya matarajio kwamba angelifanya hivyo wakati wa X’masi.