1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Wademokrats wapinga mpango wa Petraeus

13 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQ9

Nchini Marekani,wabunge wa chama cha Demokrats wameupinga mpango wa kamanda wa majeshi ya Marekani nchini Irak,Jemadari David Petraeus. Wabunge hao wamesema,mapendekezo yaliyotolewa na jemadari huyo hayalingani kabisa na matakwa ya umma.Petraeus amependekeza kuwa hadi ifikapo katikati ya mwaka 2008,vikosi vya Marekani nchini Irak vipunguzwe kwa kiasi ya wanajeshi 30,000. Harry Reid aneongoza wabunge wa Demokrats walio wengi katika Seneti amesema,wakati umewadia kufanya mabadiliko.

Kwa mujibu wa mpango wa Petraeus,Marekani itabakisha nchini Irak kama wanajeshi 130,000 hiyo ikiwa ni sawa na ile idadi iliyokuwepo kabla ya vikosi zaidi kupelekwa kati ya mwezi wa Februari na Juni.