WASHINGTON: Uingereza kuwaondoa wanajeshi wake kutoka Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 21.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Uingereza kuwaondoa wanajeshi wake kutoka Irak

Ikulu ya white house nchini Marekani imethibitisha ripoti kwamba waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair anajiandaa kutangaza tarehe ya kuanza kuwaondoa wanajeshi wa Uingereza kutoka Irak.

Msemaji wa ikulu ya Marekani mjini Washington amesema Blair alimtaarifu rais George W Bush kuhusu dhamira zake kwa njia ya simu mapema jana.

Ripoti zilizotolewa na vyombo vya habari nchini Uingereza zinasema wanajeshi 3,000 wa Uingereza wataondoka Irak kufikia mwisho wa mwaka huu, huku nusu kati yao wakirejea Uingereza katika kipindi cha wiki chache zijazo.

Msemaji wa ofisi ya waziri mkuu amesema Tony Blair atazungumzia mpango huo bungeni hii leo. Uingereza ina wanajeshi 7,000 nchini Irak, wengi wao wakiwa katika mji wa kusini wa Basra na vitongoji vyake.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com