1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Uchaguzi wa bunge wafanyika leo nchini Marekani

7 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvC

Nchini Marekani, warepublikan na wademokrate walikamilisha jana kampeni yao ya uchaguzi wa bunge ambao unafanyika baadae leo kwa majira ya Afrika ya kati na ya mashariki. Rais George W. Bush, alifanya kampeni yake ya mwisho katika majimbo ya Florida, Texas na Arkansas kusini mwa nchi. Wademokrate wanatumai kutumia hasira ambayo imezidi kupanda miongoni mwa raia kuhusu sera za rais Bush nchini Irak ili kukusanya kura zaidi.

Kiongozi wa kampeni ya uchaguzi kwa ajili ya chama cha demokrate, Charles Schumer, alisema wanatumai kupata ushindi hata katika baraza la senet.

´´Kutakuwa na ushindani mkubwa. Tunakaribia kupata ushindi wa senet. Kwa sasa, hatuwezi kufungua champaign au kusherehekea, lakini tuko katika hali nzuri tu´´.

Rais George Bush, alinufaika na kampeni hiyo ya mwisho kutetea tena sera zake juu ya Irak:

´´ Hatua yangu ya kumutoa madarakani Saddam Hussein ilikuwa ni hatua nzuri na hali ni bora duniani kutokana na hilo´´.

Kura za maoni za hivi karibuni, zilionyesha kuwa wademokrate wanaweza kulidhibiti baraza la wawakilishi, ila ni vigumu kutabiri kuhusu baraza la senet.