1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Rais Sarkozy aiunga mkono Marekani kupiga vita ugaidi

8 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C795

Rais wa Ufaransa,Nicolas Sarkozy ameihakikishia Marekani kuwa nchi yake itaiunga mkono Washington kuzuia utapakaaji wa silaha za nyuklia nchini Iran na kupiga vita ugaidi duniani.Sarkozy alitamka hayo alipohotubia bunge la Marekani ambako alipokewa kwa shangwe.

Mwaliko wa kuhotubia bunge unatazamwa kama ni ishara kuwa uhusiano kati ya Ufaransa na Marekani unakuwa bora.Rais wa zamani wa Ufaransa,Jacques Chirac alijitenga na Bush wazi wazi,kuhusu vita vya Irak.