WASHINGTON: Rais Bush aonya juu ya kuyaondoa majeshi ya Marekani kwa haraka kutoka Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 16.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Rais Bush aonya juu ya kuyaondoa majeshi ya Marekani kwa haraka kutoka Irak

Rais George W Bush wa Marekani ameonya juu ya kuwaondoa wanajeshi wa Marekani kwa haraka kutoka Irak akisema kufanya hivyo kutauhatarisha usalama wa kitaifa wa Marekani.

Rais Bush amesema hatua hiyo itawapa nguvu magaidi na kundi la al Qaeda litapata fursa ya kusajili wanachama wapya na kupata ngome mpya.

Kiongozi huyo ameongeza kusema kwamba Irak iliyo huru italinyima kundi la al-Qaeda maficho na kuzuia njama za uharibifu za Iran.

Rais Bush pia amesema Irak itakuwa mshirika muhimu katika vita dhidi ya ugaidi.

Rias Bush ameyasema hayo baada ya maelfu ya waandamanaji waliokuwa na hasira, wakiwemo pia jamaa za wanajeshi wa Marekani waliouwawa nchini Irak, kufanya maandamano mjini Washington wakitaka vita nchini Irak vimalizike, wanajeshi wa Marekani warejee nyumbani na rais Bush ashtakiwe.

Waandamanaji 150 wamekamatwa na polisi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com