WASHINGTON: Mwanafunzi wa tano amefariki dunia nchini Marekani kufuatia shambulio kwenye shule | Habari za Ulimwengu | DW | 03.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Mwanafunzi wa tano amefariki dunia nchini Marekani kufuatia shambulio kwenye shule

Wanafunzi wengine wawili wamefariki dunia miongoni mwa waliyojeruhiwa katika shambulio dhidi ya shule mmoja katika jimbo la Pennsylvania nchini Marekani na kufikisha idadi ya watu watano waliyouawa na mtu aliyekuwa na bunduki. Mtu huyo kwa jina Charles carl Roberts wa IV mwishoni mwa wiki aliwateka nyara wanafunzi kutoka jamii ndogo ya Amish katika kijiji cha Paradise na kuwauwa wasichana watatu baada ya kuwaachilia huru wavulana wote na kwisha kujiuawa kwa risase.

Shambulio hilo ni na tatu lililolenga shule na kusababisha mauwaji kwa muda wa wiki mmoja tu. Polisi wanafanya uchunguzi kuhusu taarifa kwamba kitendo hicho cha mauwaji kilijkuwa cha ulipizaji kisase kwa yale yaliyotokea miaka 20 iliyopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com