WASHINGTON : Muswada wa kugharamia vita wapita | Habari za Ulimwengu | DW | 23.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON : Muswada wa kugharamia vita wapita

Nchini Marekani jopo la baraza la senate la bunge la Marekani limeidhinisha dola bilioni 122 kugharamia vita nchini Iraq na Afghanistan lakini pia limemkaidi Rais George W. Bush wa Marekani kwa kumtaka kuwaondowa wanajeshi wake kutoka Iraq ifikapo mapema mwakani.

Ikulu ya Marekani imetishia kuupigia kura ya turufu muswada huo.

Wabunge wa chama cha Demokrat wamesema lugha iliotumika kwenye muswada huo yenye kutaka kuondolewa kwa wanajeshi hao ni muhimu katika kuilazimisha serikali ya Iraq kuwajibika zaidi.

Muswada huo unataka vikosi vya Marekani kuanza kuondoka Iraq katika kipindi kisichozidi miezi minne baada ya kupitishwa kwake na kuweka tarehe isio ya kushurutisha ya kutaka kuondolewa kwa vikosi vyake vya mapigano ifikapo tarehe 31 mwezi wa Machi mwaka 2008.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com