1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON : Muswada kuondowa wanajeshi Iraq wapita

Baraza la wawakilishi la bunge la Marekani lililogawika limeweka kando tishio la kura ya turufu na kupistisha muswada wa sheria ambao utamuamuru Rais George W.Bush kuanza kuondowa vikosi vya Marekani kutoka Iraq kuanzia tarehe Mosi Oktoba.

Muswada huo uliopita kwa kura 218 dhidi ya 208 leo hii umekuja wakati kamanda mkuu wa majeshi ya Marekani nchini Iraq akiwaamabia wabunge kwamba nchi hiyo bado imo kwenye umwagaji damu lakini kuna dalili fulani za hali kuwa nzuri.

Muswada huo baada ya kuvuka bungeni mwishoni mwa wiki hii na kuwasili kwenye meza ya rais siku chache ziijazo ni changamoto ya kwanza ya bunge yenye kushurutisha kwa namna Bush anavyoushughulikia mzozo wa Iraq ambao sasa uko katika mwaka wake wa tano.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com