WASHINGTON: Mswada wa sheria wataka vikosi viondoshwe Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 13.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Mswada wa sheria wataka vikosi viondoshwe Irak

Baraza la Wawakilishi nchini Marekani,limepitisha mswada wa sheria unaotoa wito wa kuondosha baadhi kubwa ya vikosi vya Marekani kutoka Irak,kuanzia kipindi cha siku 120 zijazo na hatua hiyo ikamilishwe ifikapo tarehe mosi Aprili.Mswada huo umepitishwa kwa kura 223 dhidi ya 201 zilizopinga.Wakati wa mdahalo,viongozi wa chama cha Demokratik walisema,sera za vita za Bush zimeshindwa na sasa ni wakati wa kuchukua hatua tofauti.Spika katika Baraza la Wawakilishi,Bibi Nancy Pelosi amesema:

„Vita nchini Irak ni kipingamizi kwa juhudi za kupambana kikamilifu dhidi ya ugaidi,hasa nchini Afghanistan na maeneo mengine.Kwa sheria hii mpya,tunachukua hatua kubwa ya kuvimaliza vita hivyo.“

Hata hivyo,sheria hiyo inakabiliwa na kura ya turufu ya rais George W.Bush aliekwishasema kuwa hatotia saini mswada wowote utakaopanga ratiba ya kuviondosha vikosi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com