1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Mpango wa Bush kwa Iraq washutumiwa

12 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbV

Wabunge wa Marekani wameushutumu vikali uamuzi wa Rais George W. Bush wa kuepelea wanajeshi wa zaida wa Marekani zaidi ya 20,000 nchini Iraq.

Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Nje ya baraza la senate la bunge la Marekani wa chama cha Demokrat Joe Biden ameulezea mpango huo kuwa ni kosa la kusikitisha.

Seneta wa chama cha Republican Chuck Hagel amesema itakuwa ni kuboronga vibaya sana kwa sera ya kigeni kuwahi kufanyika tokea vita vya Vietnam.Kauli hizo zinakuja wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Condoleezza Rice akitetea mkakati mpya wa Rais Bush juu ya suala la Iraq ambapo amesema litakuwa ni jukumu la Iraq kuhakikisha kwamba mpango huo unafanikiwa.

Waziri wa Ulinzi Robert Gates ameieleza Kamati ya Huduma za Kijeshi ya Baraza la Wawakilishi la bunge la Marekani kwamba iwapo serikali ya Marekani haitotimiza wajibu huo kwa upande wake vikosi hivyo vya ziada yumkini visipelekwe.