1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Misaada zaidi kwa nchi masikini

28 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBM3

Benki ya Dunia itaongeza kwa maradufu msaada unaotolewa kwa nchi masikini kabisa duniani. Mikopo na misaada ya Dola bilioni tatu na nusu itatolewa kati ya mwaka 2008 na 2010.Mradi wa miaka mitatu iliyopita,uligharimu Dola bilioni moja na nusu.Rais mpya wa Benki Kuu ya Dunia, Robert Zoellick amesema,wafadhili wanatakiwa kusaidia zaidi,nchi 81 zilizo masikini kabisa duniani.