1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Maseneta kupinga bungeni mpango wa Rais George W. Bush kuhusu Iraq

18 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZl

Kundi la maseneta wa Marekani akiwemo mbunge wa Republican anayepinga vita vya Iraq, limekubaliana kuwasilisha muswada bungeni kupinga mpango wa Rais George W. Bush kupeleka wanajeshi wa ziada elfu ishirini na moja nchini Iraq.

Muswada huo ambao unatarajiwa kuwasilishwa bungeni mapema juma lijalo unasisitiza kwamba vita vya Iraq haviendeshwi kwa manufaa ya Marekani.

Hata hivyo, msemaji wa Rais George Bush amesema miswada yoyote italayopitishwa bungeni haitaathiri uamuzi wa rais.

Nchini Iraq, Waziri Mkuu, Nuri Al-Maliki alikutana na mabalozi wa mataifa ya kigeni na kueleza lengo na serikali yake kurejesha usalama nchini humo.

Nuri Al-Maliki aliyelekea kujibu shutuma dhidi ya utendaji kazi wa serikali yake alisema:

O TON MALIKI

„Serikali yetu imepania kuimarisha uhusiano wa kisiasa pamoja na mataifa mengine. Kusema la haki, hali ya usalama ndio changamoto kubwa kwetu. Tunazingatia sana suala hilo kwani tukifanikiwa kurejesha usalama, sekta nyingine zitaimarika kwa kiasi kikubwa“

Huku hayo yakiendelea, nchini Iraq mashambulio kadhaa ya mabomu yametokea mjini Baghdad na kusababisha vifo vya watu kumi na saba.

Afisa wa usalama wa Iraq amesema wanamgambo wameripua mabomu matano yaliyosababisha pia watu takriban hamsini kujeruhiwa.