1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Marekani yaamuru uchunguzi Guantanamo

15 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2l

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imeamuru kufanyika uchunguzi juu ya madai ya hivi karibuni kabisa ya mateso katika gereza la kijeshi la Marekani huko Guantanamo nchini Cuba.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Tony Show amesema amri hiyo imetolewa baada ya mwanamaji wa kike wa cheo cha sajent wa Marekani kusema kwamba aliwahi kuwasikia walinzi katika kituo hicho cha mahabusu wakijigamba juu ya kuwatesa kimwili na kiakili wafungwa wanaoshikiliwa huko.

Marekani bado ingali inawashikilia takriban watuhumiwa 400 huko Guantanamo licha ya wito wa kimataifa wa kutaka kufungwa kwa kambi hiyo.