1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Marekani na Ujerumani zataka majadiliano zaidi juu ya mpango wa ulinzi dhidi ya makombora.

20 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHM

Katika ziara yake mjini Washington , waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amesema kuwa mpango wa Marekani wa kujenga ngao ya ulinzi dhidi ya makombora katika bara la Ulaya hauharibu uhusiano na Marekani.

Wakati Ujerumani na Marekani zinatafuta kutuliza hali kuhusu uhusiano wao, waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amesema kuwa mfumo huo wa ulinzi dhidi ya makombora utakuwa na hali ya kuleta uimara katika bara la Ulaya.

Amesema kuwa Marekani inaendeleza mashauriano na washirika wake wa Ulaya pamoja na Russia, nchi ambayo moja kwa moja inapinga mipango hiyo.

Steinmeier amesema anaimani kuwa Marekani inauelewa wito wa kansela wa Ujerumani Angela Merkel wa majadiliano wazi ya pande zote ya kuhusu suala hilo.