WASHINGTON : Marekani kuuwa majasusi wa Iran walioko Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 26.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON : Marekani kuuwa majasusi wa Iran walioko Iraq

Jeshi la Marekani limeagizwa kuuwa au kuwateka makachero wa Iran wanaoendesha shuguli zao za ujasusi nchini Iraq.

Gazeti la Washington Post limeripoti hayo hapo Ijumaa.

Repoti hiyo imetaja maafisa isiowataja majina wa serikali na wale wa kupiga vita ugaidi wenye taarifa za moja kwa moja juu ya mpango huo.Sera hiyo ambayo inatumika kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa inawahusu mashushu wa ujasusi wa Iran na wanajeshi wa Kikosi cha Mapinduzi cha Iran ambao inadhaniwa kuwa wanashirikiana na wanamgambo wa Iraq lakini haiwahusu raia au wanadiplomasia.

Kwa mujibu wa repoti hiyo kwa zaidi ya mwaka mmoja vikosi vya Marekani vimekuwa vikiwashikilia madarzeni ya Wairan na kuchunguza baadhi ya sampuli zao za DNA chembe hai za urithi pamoja na kuwapiga picha na kuchukuwa alama zao za vidole.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com