1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Mareakani kutaka azimio jipya dhidi ya Iran

23 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCPW

Msaidizi waziri wa mambo ya nje wa Marekani Nicholas Burns amesema mataifa matano wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani yatakutana kujadili mpango wa nuklea wa Iran mjini London hapo Jumatatu.

Burns amewaambia waandishi wa habari mjini Washington kwamba Marekani itataka rasimu ya azimio jipya la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuitenga Iran kwa kushindwa kutimiza agizo la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa siku ya mwisho iliotakiwa kusitisha urutubishaji wa uranium.

Burns alikuwa akizungumza masaa mchache tu baada ya shirika linaloshughulikia masuala ya nuklea la Umoja wa Mataifa kutowa repoti inayosema kwamba sio tu Iraan imepuuza muda wa kutekeleza agizo hilo bali pia imekuwa ikiuharakisha mpango wake huo wa nuklea.

Baraza la Usalama linahofu kwamba Iran yumkini ikawa inataka kutengeneza silaha za nuklea wakati Iran yenyewe ikikanusha kwamba mpango wake huo wa nuklea ni kwa ajili ya dhamira za amani tu.