1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Maoni mbalimbali yatolewa kuhusu mkakati mpya wa Rais George W Bush nchini Iraq.

11 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbc

Uingereza, Australia na Japan zimeunga mkono mpango wa Rais wa Marekani, George W. Bush , wa kuongeza idadi ya majeshi nchini Iraq.

Hata hivyo, nchi hizo hazikusema endapo zitaisadia Marekani, kijeshi.

Rais George Bush alizindua mkakati mpya wa serikali yake nchini Iraq kwa hotuba kupitia televisheni akipendekeza kuongezwa kwa wanajeshi zaidi ya elfu ishirini nchini humo.

Wabunge wa chama cha Demokratic wameyapinga mapendekezo ya Rais Bush wakisema yatachochea zaidi mzozo huo.

Seneta wa Jimbo la Illinois, Barak Obama wa chama cha Democratic, ameizungumzia hotuba ya Rais George Bush.

O TON OBAMA

„Sikusikia lolote katika hotuba hiyo linalothibitisha hatua ya kuongeza wanajeshi elfu kumi na tano au elfu ishirini wa Marekani nchini Iraq kwamba itasaidia kuzima ghasia za kimadhehebu. Sikumsikia akitaja sera yoyote ya kisiasa itakayowasaidia wananchi wa Iraq kushirikiana kisiasa“

Nchini Ujerumani mratibu wa serikali wa uhusiano na Marekani, Karsten Voigt, amezitilia shaka taratibu hizo mpya. Karsten Voigt ameahidi serikali itazishawishi Syria na Iran zishiriki katika juhudi za kibalozo kuisaidia Iraq.