1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Mama Pelosi ashika wadhifa wa Spika

5 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdG

Nchini Marekani Nancy Pelosi amekuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kwenye wadhifa wa spika wa Baraza la Wawakilishi la bunge la Marekani.

Mbunge huyo wa chama cha Demokrat wa jimbo la Carlifonia alishinda kwa kura 223 dhidi ya 202.Pelosi alipokea nyundo ya spika kutoka kwa mbunge wa baraza hilo John Boehner ambaye hivi sasa anakuwa kiongozi wa wabunge wachache kwenye baraza hilo la bunge.Nafasi hiyo inamfanya ashikilie wadhifa wa juu kabisa kushikiliwa na mwanamke katika historia ya serikali ya Marekani.

Pelosi ameshika wadhifa huo wa Uspika baada ya chama cha Demokrat kushika udhibiti wa bunge la Marekani kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha miaka 12.

Chama hicho cha Demokrat kilinyakuwa ushindi katika uchaguzi wa bunge wa mwezi wa Novemba kwa kutumia fursa ya kukatishwa tamaa kwa wanananchi wa Marekani kutokana na jinsi utawala wa Rais Bush unavyoshughulikia vita vya Iraq.