1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Majadiliano ya pande sita yafanywa juma lijalo

15 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPh

Mpatanishi mkuu wa Marekani katika majadiliano ya Korea ya Kaskazini amearifu kuwa mazungumzo ya nchi sita kuhusu miradi ya kinyuklia ya Pyongyang,yataanza tena juma lijalo.

Naibu-Waziri wa Nje wa Marekani,Christopher Hill amesema,wapatanishi wa nchi hizo sita:Marekani, Urusi,China,Japani na Korea zote mbili, wanatazamiwa kujadili njia za kuufunga mtambo wa nyuklia wa Korea ya Kaskazini.

Pyongyang,kimsingi imekubali kusitisha miradi yake yote ya nyuklia,kama sehemu ya maafikiano yaliopatikana mwezi wa Februari kati ya nchi hizo sita.