1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Maandamano kupinga ubaguzi wa rangi

21 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBO0

Nchini Marekani,maelfu ya watu wameandamana katika mji wa Jena kwenye jimbo la Louisiana kupinga ubaguzi wa rangi.Maandamano hayo yamefanywa kulalamika kuhusu mashtaka ya uhalifu yaliyotolewa dhidi ya wanafunzi sita weusi waliompiga na kumjeruhi mwanafunzi mweupe katika ugomvi uliotokea shuleni katika mji mdogo wa Jena.Wanafunzi hao sita wamefikishwa mahakamani. Wafanya maandamano wanasema,kesi hiyo ni ishara ya sheria inayobagua weusi.