WASHINGTON: Maalfu waandamana kupinga vita vya Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 18.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Maalfu waandamana kupinga vita vya Irak

Maalfu ya watu wamefanya maandamano kupinga vita vya nchini Irak vinavyoingia katika mwaka wa nne baada ya majeshi ya Marekani kuivamia nchi hiyo kwa kushirikiana na nchi kadhaa.

Maalfu ya wapinga vita hao hawakujali baridi kali mjini Washington ili kupinga vita hivyo wakiwa wamebeba mabango juu ya kuvishutumu vita hivyo.

Jumanne ijayo, utatimu mwaka wa nne tokea vita hivyo vianze ambapo maalfu ya wairaki na askari alfu3 na mia 2 wa Marekani wameuawa.

Maandamano mengine yalifanyika katika miji kadhaa ya Marekanai ikiwa pamoja na Los Angeles, katika miji ya Ulaya na Australia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com