Washington. IMF yapata mkurugenzi mpya. | Habari za Ulimwengu | DW | 29.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Washington. IMF yapata mkurugenzi mpya.

Shirika la fedha la kimataifa IMF limemteua Dominique Strauss Kann kuwa mkuu wake jana Ijumaa wakati taasisi hiyo inahitaji kujiangalia binafsi kutokana na shaka shaka dhidi yake duniani kote.

Bodi ya utendaji wa shirika hilo imesema kuwa imemchagua kwa maridhiano waziri wa zamani wa fedha wa Ufaransa kuwa mkurugenzi mkuu kwa kipindi cha muda wa miaka mitano, kuanzia Novemba mosi, akichukua nafasi ya Rodrigo Rato raia wa Hispania .

Strauss-Kann amesema katika taarifa baada ya tangazo la kuchaguliwa kwake kuwa ana nia ya kusukuma bila kuchelewa mageuzi yanayohitajika katika shirika la IMF ili kuweka uthabiti wa fedha.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com