1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Gates asema matamshi ya Putin yasumbua

27 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7CJ

Waziri wa Ulinzi wa Marekani,Robert Gates amesema matamashi yaliyotolewa hivi karibuni na Rais wa Urusi,Vladimir Putin kuhusu mradi wa Marekani kuweka makombora ya kujihami katika Ulaya ya Mashariki yanasumbua.

Rais Putin,kwenye mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya na Urusi nchini Ureno,alifananisha mgogoro wa makombora wa hivi sasa na mzozo wa makombora wa Kuba,uliozuka mwaka 1962.Wakati huo,Marekani na Urusi zilikuwa ukingoni mwa vita vya nyuklia.