WASHINGTON: El-Marsi anasema Marekani iombe msamaha
30 Novemba 2006Matangazo
Mjerumani mwenye asili ya Kilebanon El -Masri anaitaka Marekani iombe msamaha kwa sababu ya kutekwa nyara na mawakala wa shirika la kijasusi la Marekani CIA.Baada ya kukutana na wajumbe wa Seneti ya Marekani mjini Washington,El-Masri alisema anataka kuelezwa kwanini alitendewa hivyo.