WASHINGTON: Cheney ampongeza marehemu Ford | Habari za Ulimwengu | DW | 31.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Cheney ampongeza marehemu Ford

Wabunge wa Marekani wamekusanyika kwa mazishi ya kitaifa ya rais wa zamani wa Marekani Gerald Ford. Makamau wa rais wa Marekani, Dick Cheney, amempongeza marehemu Ford kwa kumsamehe rais aliyemtangulia Richard Nixon na kusaidia Marekani kuondokana na athari za kashfa ya Watergate.

Gerald Ford aliyekuwa mbunge wa chama cha Republican kwa miaka 25, alikuwa rais wa Marekani kuanzia mwezi Agosti mwaka wa 1974 hadi Januari mwaka 1977.

Ford alichukua nafasi iliyowachwa na rais Richad Nixon aliyejiuzulu kufatia kashfa ya Watergate. Ford alifariki dunia mnamo Jumanne wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 93. Atazikwa Jumatano ijayo huko Grand Rapids, Michigan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com