1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush kuzuia uhamiaji haramu kwa milele

23 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpE

Rais George W.Bush ameapa kupiga marufuku kwa milele wahamiaji wanaoingia Marekani kwa njia zisizo halali.Bush amezindua mpango mpya wa mageuzi kuhusu uhamiaji,baada ya juhudi ya kwanza kushindwa kupata kura za kutosha bungeni.Hata hivyo lakini,ajenda hiyo mpya inakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka wabunge wa Republikan na Demokrat.Wabunge hao wanasema,kuwapa hadhi halali,wahamiaji kama milioni 12 ambao hivi sasa tayari wanaishi Marekani kinyume na sheria, kutavutia watu zaidi kujipenyeza kwenye mpaka wa Mexico ambao ni vigumu sana kulindwa.