1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush atoa mwito wa kurejesha demokrasia Pakistan

6 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79c

Rais wa Marekani,George W.Bush kwa mara ya kwanza ametamka rasmi kuhusu amri ya hali ya hatari iliyotangazwa nchini Pakistan.Akizungumza mjini Washington,Bush ametoa mwito kwa mshirika wake Jemadari Pervez Musharraf kurejesha demokrasia haraka,kufanya uchaguzi kama ilivyopangwa hapo awali na ajiuzulu kama mkuu wa majeshi.Lakini Bush hakutamka cho chote juu ya suala la kusitishwa msaada wa fedha kwa Pakistan.

Hapo awali mjini Lahore,polisi walitumia marungu na mabomu ya kutoa machozi dhidi ya mamia ya wanasheria waliokuwa wakiandamana.Tangu amri ya hali ya hatari kutangazwa siku ya Jumamosi,zaidi ya watu 1,500 wametiwa mbaroni.Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier amesema, serikali imeingiwa na wasiwasi kuhusika na ripoti kuwa majaji na viongozi wa upinzani wametiwa ndani.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon ametoa mwito kwa Musharraf kuwaachilia huru wote waliotiwa ndani.