1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Bush akubali kuondowa vikosi kwa awamu

14 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPs

Rais George W. Bush wa Marekani akitetea vita vya Iraq ameamuru hapo jana usiku kupunguzwa kwa wanajeshi wa Marekani walioko Iraq kwa awamu ambapo amesema kwa kadri watakavyofanikiwa ndivyo wanajeshi zaidi wa Marekani watakavyoweza kurudi nyumbani.

Lakini hata hivyo Bush bado ingali anakataa kabisa wito wa kumaliza vita vya Iraq kwa kusema kwamba waasi ambao wanatishia mustakbali wa Iraq ni tishio kwa usalama wa taifa wa Marekani.

Bush amesema vikosi vya Marekani lazima viendelee kubakia kwenye mapambano na zaidi ya wanajeshi 130,000 wataendelea kubakia nchini humo baada ya amri mpya ya kuwaondowa itakapokuwa imekamilika hapo mwezi wa Julai.