1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bodi kuamua hatima ya Wolfowitz

15 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1r

Rais wa Benki ya Dunia,Paul Wolfowitz alikwenda kinyume na sheria na maadili ya benki hiyo alipochukua hatua ya kuongeza mshahara na kumpandisha cheo mpenzi wake miaka miwili iliyopita.Hayo ni matokeo ya ripoti ya jopo maalum lililoteuliwa kuchunguza kashfa hiyo. Ripoti ya jopo hilo pia inashauri kuwa bodi ya Benki Kuu yenye nchi wanachama 24 lazima izingatie ikiwa Wolfowitz ataweza kuendelea kuiongoza benki hiyo kwa ufanisi.Lakini Wolfowitz alie na umri wa miaka 63,anapinga kufanya makosa yo yote yale.Hatima yake itaamuliwa baadae leo hii atapokutana na bodi ya wakurugenzi wa Benki Kuu mjini Washington.