1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Baraza la wawakilishi laidhinisha fedha za vita kwa mafungu.

11 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC39

Baraza la wawakilishi nchini Marekani limepiga kura kugharamia vita vya Iraq kwa mafungu katika muda wa miezi michache ijayo.

Rais George W. Bush ametishia kupinga muswada huo kwa kura ya turufu. Baraza hilo la wawakilishi limeidhinisha dola bilioni 43 ikiwa ni gharama za dharura kwa ajili ya vita nchini Iraq na Afghanistan, lakini rais Bush anatakiwa kuonyesha hatua za maendeleo zilizopigwa katika kuiimarisha Iraq hadi ifikapo mwezi Julai.

Wabunge hao baada ya hapo wataamua iwapo nyongeza ya dola bilioni 53 itumike kuendeleza mapambano ama kuwarejesha wengi wa wanajeshi wa Marekani nyumbani kutoka Iraq.

Spika wa baraza hilo la wawakilishi Nancy Pelosi kutoka chama cha Democratic amesema kuwa kura iliyopigwa jana Alhamis imemaliza kile alichokiita hundi ya wazi kwa rais kwa ajili ya vita, lakini rais Bush ameieleza sheria hiyo kuwa isiyo na mpango na ya mafungu.