WASHINGTON: Al-Maliki anaunga mkono mradi mpya wa Bush | Habari za Ulimwengu | DW | 19.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Al-Maliki anaunga mkono mradi mpya wa Bush

Ikulu ya Marekani imepuuza madai ya waziri mkuu wa Irak kuwa vikosi vya Kiiraki havikupatiwa silaha kwa haraka na Marekani.Katika matamshi yaliyochapishwa kwenye magazeti ya Marekani na Uingereza,waziri mkuu Nouri al-Maliki amesema haja ya kuwa na vikosi vya Kimarekani nchini Irak itapunguka sana katika muda wa miezi mitatu hadi sita,ikiwa Marekani itaharakisha kulipatia silaha jeshi la Irak.Msemaji mkuu wa rais George W.Bush wa Marekani,Tony Snow amesema,al-Maliki ametamka fikra hiyo mara kadhaa na ameeleza kuwa ukosoaji huo umesababishwa na hali ya kutofahamiana. Akaongezea kuwa al-Maliki anakubaliana kabisa na sera mpya ya Bush kuhusu Irak,ambayo ilitangazwa juma lililopita ikiwa ni pamoja na kupelekwa zaidi ya wanajeshi 20,000 wengine wa Kimarekani nchini Irak.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com