WASHINGTON: Afisa wa jeshi la Marekani afikishwa mahakamani | Habari za Ulimwengu | DW | 20.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Afisa wa jeshi la Marekani afikishwa mahakamani

Afisa pekee wa jeshi la Marekani anayekabiliwa na kesi ya mateso ya wafungwa katika jela ya Abu Ghraib nchini Irak atafikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi ya Fort Meade, Maryland nchini Marekani hii leo.

Zaidi ya miaka mitatu tangu picha za mateso ya wafungwa wa Irak zilipowashutua walimwengu, ni wanajeshi 11 pekee wa Marekani walioshtakiwa, lakini hakuna afisa yeyote wa ngazi ya juu katika jeshi la Marekani aliyewahi kufunguliwa mashitaka.

Wanajeshi hao walihukumiwa vifungo kati ya saa chache za kufanya kazi katika jamii hadi miaka kumi gerezani. Wengi wao wanasema walikuwa wakifuata amri kutoka kwa wakubwa wao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com