Warusi wanataka Ahtisaari asishughulikie tena suala la Kosovo | Habari za Ulimwengu | DW | 18.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Warusi wanataka Ahtisaari asishughulikie tena suala la Kosovo

Moscow:

Urusi imetamka wazi kabisa mjumbe maalum wa umoja wa mataifa kuhusu Kosovo Martti Ahtisaari hastahiki kuendelea na wadhifa huo.Mwenyekiti wa baraza la usalama la Urusi Igor Ivanov amenukuliwa na shirika la habari la nchi hiyo-Interfax akisema “hakuna dalili za kufikia maridhiano kuhusu pendekezo la Ahtisaari,kuhusu mustakbal wa Kosovo.Ndio maana panahitajika duru nyengine ya majadiliano yatakayoongozwa na mjumbe mwengine wa Umoja wa mataifa”-limeandika shirika la habari la interfax likimnukuu Igor Ivanov.Matamshi kama hayo yalitolewa jana na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi Sergej Lawrow.Waserbia wanapinga pendekezo hilo linalozungumzia juu ya kupatiwa madaraka makubwa kupita kiasi jimbo hilo la Serbia linaloongozwa na Umoja wa mataifa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com