1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WAR SAW:Urussi yadaiwa kuweka sheria kali kwa waangalizi wa uchaguzi ujao

1 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7At

Shirika la usalama na ushirikiano baranai Ulaya limesema Urussi imeweka sheria za aina yake kwa waangalizi katika uchaguzi ujao wa bunge nchini humo.

Msemaji wa shirika hilo la OSCE amefahamisha kwamba serikali ya mjini Moscow imepunguza idadi ya waangalizi kwa thuluthi mbili ikilinganiswa na waliosimamia uchaguzi huo mwaka 2003

Aidha Urussi imetaka kufanya uamuzi juu ya kundi litakalowakilisha shirika hilo la OSCE katika uchaguzi.

Hatua hiyo ya Urussi imekosolewa pia na Marekani ambapo msemaji wa Ikulu ya White House ameitaja hatua ya Urussi kuwa yenye kusababisha wasiwasi.